SmartCard

Bei

Bei moja, wazi. Kila kitu ndani.

Unalipa kwa kila kadi unayotuma, si kifurushi usichokitumia. Kadi 20 za kwanza za kila tukio ni bure, na michango ni bure kabisa.

Unatengeneza mwenyewe

SmartCard

TSh 1,200kwa kadi

Kadi 20 za kwanza bureKadi 500+: TSh 1,000 kila moja

Chagua muundo, weka wageni na tuma ndani ya dakika chache, kutoka kwenye simu yako.

  • Miundo yote ya kadi, Kiswahili au Kiingereza
  • WhatsApp bila kikomo, bila malipo
  • SMS 3 kwa kila kadi: mwaliko, ukumbusho na shukrani
  • Majibu ya wageni (RSVP) moja kwa moja
  • QR mlangoni na wasaidizi wako wa mlangoni
  • Michango, ahadi na vikumbusho

Inayopendwa zaidi

Tunakufanyia

SmartCard Plus

TSh 2,000kwa kadi

Timu yetu inabuni kadi yenu, inaingiza orodha ya wageni na kutuma kwa niaba yenu.

  • Kila kitu kilicho kwenye SmartCard
  • Muundo maalum wa kadi yenu, marekebisho 2
  • Tunaingiza orodha ya wageni na kutuma
  • SMS 6 kwa kila kadi
  • Kadi ya save-the-date
  • Kampeni ya SMS ya michango
  • Tayari ndani ya saa 48

Huduma kamili

SmartCard Kamili

TSh 3,000kwa kadi

Kwa familia zinazotaka mtu mmoja wa kufuatilia kila kitu hadi siku ya sherehe.

  • Kila kitu kilicho kwenye Plus
  • SMS 10 kwa kila kadi
  • Tunawapigia simu wageni ambao hawajajibu
  • Msimamizi maalum kwenye WhatsApp
  • Ripoti ya mwisho ya mahudhurio na michango

Kokotoa gharama yako

Weka idadi ya kadi utakazotuma. Kadi ya watu wawili (double) ni kadi moja.

Hakuna gharama zilizofichwa. SMS za ziada ni TSh 35 kila moja.

Jumla

SmartCard
TSh 336,000TSh 1,120 × 300
SmartCard Plus
TSh 600,000TSh 2,000 × 300
SmartCard Kamili
TSh 900,000TSh 3,000 × 300

Kila kifurushi kina

  • WhatsApp bure

    Tuma kadi kutoka simu yako kwa kubofya mara moja.

  • Michango bure

    Anza kukusanya ahadi miezi kabla, hata kabla ya kununua kadi.

  • QR mlangoni

    Kila mgeni anaingia na idadi ya watu wa kadi yake tu.

  • Saa za Kiswahili

    Kila kadi inaonyesha saa kama "saa 10 jioni".

Maswali kuhusu malipo

Kadi moja ni nini?

Ni mwaliko mmoja kwa mgeni au familia, hata kama inaruhusu watu wawili au zaidi. Unalipa kwa kadi, si kwa kila mtu.

Nalipaje?

Kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa. Unalipia kadi kabla ya kuzituma, na unaweza kuongeza kadi wakati wowote orodha inapokua.

Kadi 20 za bure zinafanyaje kazi?

Kila tukio kwenye kifurushi cha SmartCard linapata kadi 20 za kwanza bure. Sherehe ndogo ya wageni 20 au chini haina gharama kabisa.

SMS zikiisha?

Kila kadi ina SMS zake. Ukihitaji zaidi, kwa mfano vikumbusho vya michango, kila SMS ya ziada ni TSh 35. WhatsApp inabaki bure.

Nikibadilisha taarifa baada ya kutuma?

Kadi ni ukurasa hai: ukibadilisha ukumbi au saa, wageni wote wanaona taarifa mpya kwenye kiungo kile kile, bila kulipa tena.

Karibu tusherehekee pamoja

Anza leo, lipa unapotuma.

Anza bure

Kwa waandaaji wa sherehe

Unaandaa sherehe nyingi kwa mwaka? Pata bei maalum kwa vifurushi vya matukio, dashibodi ya matukio yote na msaada wa WhatsApp wa haraka.